27 Agosti 2013 - 19:30
Vita baridi dhidi ya Syria

Vyombo vya kimagharibi vya tangaza vita dhidi ya Syria kueleza kuwa Syria itavamiwa mnamo siku chache za usoni.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Marekani na wanaomuunga mkono wameanza kutangaza vita dhidi ya Syria katika vyombo vyao vya habari kueleza kuwa utawala wa Syria umefika mwisho mnamo siku kadhaa Syria itavamiwa na Marekani wakishirikia na Mfaransa, Muigereza na Saudia Arabia.

Vyombo hivyo vya kimagharibi havikutosheka tu kwa propaganda zake za kufamiwa Syria bali vilionyesha ndege za kivita, manwari na jeshi kubwa likijiandaa na vita dhidi ya Syria.

Mzozo wa Syria umekuwa ni gumzo katika nchi za kimagharibi kushindwa wafanye nini kwa kila siku kwa zuka madai mapya kunako waasi wa Syria.